MTANGAZAJI

CHANGAMOTO ZA UVIKO 19 NA ONGEZEKO LA WA ADVENTISTA DUNIANI

  


Zaidi ya watu milioni 1 walijiunga na Kanisa la Wa Adventista wa Sabato katika mwaka  2021, kwa mujibu wa data kutoka Ofisi ya Kumbukumbu, Takwimu na Utafiti ya Kanisa hilo (ASTR).

Mkurugenzi wa ASTR Dkt David Trim, ameeleza  kwenye mkutano wa Mkuu wa 61 wa Konferensi Kuu ulimalizika hivi karibuni kuwa idadi ya waumini walioandikishwa  imeonesha kuongezeka tena mwaka  2021 baada ya kupungua sana wakati wa janga la Uviko 19.

Takwimu za ASTR zinaonesha mwaka 2004 ulikuwa ni mwaka wa kwanza kwa kipindi cha miaka 16 ambako kulikuwa na ongezeko la waumini wa wa Kanisa hilo zaidi ya milioni moja duniani lakini baada ya Uviko 19 idadi ilishuka.

Kuanzia mwaka  2019 hadi 2020 ongezeko la waumini  lilipungua kwa zaidi ya nusu-milioni, ukishuka kutoka milioni 1.32 hadi 800,000, ambayo ilikuwa jumla ya chini kabisa ya ongezeko tangu 1997. 

Japokuwa mwaka 2021, licha ya athari zinazoendelea za janga la Korona  uandikishaji uliongezeka kwa zaidi ya watu  200,000, na  kwa mara nyingine tena walikua zaidi ya milioni 1.

Licha ya idadi kubwa ya watu wanaojiunga na Kanisa, kuwahifadhi bado ni tatizo, huku Kanisa likiwa na idadi ya kubwa waumini  wanaoondoka katika miaka ya hivi karibuni.

Dkt Tim anasema hii ilikuwa kweli hasa kwa 2019 mwaka wa kwanza kabisa ambapo kulikuwa na  zaidi ya waumini milioni moja  walioliacha kanisa,huku uandikishaji na kifo ikiwa ni sababu za kushuka kwa idadi.

Takwimu hizo  zinaonesha kuwa Kanisa la Wa Adventista wa Sabato linaonesha ukuaji katika kipindi cha miaka 50 kuanzia mwaka 1970 hadi 2020,ikihusisha ukuaji katika idadi ya Union kwa asilimia 54,konferensi asilimia 98,shule za msingi asilimia 64,Shule za sekondari asilimia 570,Taasisi za Afya asilimia 500,Idadi ya Wachungaji imeongezeka kwa asilimia 142 na watumishi wengine asilimia 159

Hadi Disemba 31,2021 kwa mujibu wa  tovuti ya Kanisa la Wa Adventista wa Sabato,kulikuwa na waumini  21,912,161 wa kanisa hilo Duniani,kukiwa na makanisa 95,297.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.