MTANGAZAJI

IDADI YA WA ADVENTISTA TANZANIA ILIPUNGUA MWAKA 2020-ASTR

  


Jumla ya watu 6,218 waliliacha kanisa la Wa Adventista wa Sabato nchini Tanzania huku miongoni mwao wakiwa hawajulikani walipo,ambapo 3,805 ni kutoka katika unioni ya Kaskazini mwa Tanzania huku Unioni ya Kusini mwa Tanzania ikiwa ni watu 2,413 kwa mujibu wa data za mwaka 2020 za Ofisi ya Kumbukumbu, Takwimu na Utafiti ya Kanisa hilo duniani  (ASTR).

Takwimu hizo zinaonesha kuwa waumini wapatao 2,034 waliondolewa kwenye idadi ya waumini katika kanisa hilo baada ya kufariki dunia kutokana na sababu mbalimbali.

Tanzania ni miongoni mwa nchi 11 zinazounda Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati (ECD) yenye unioni 12 ambapo kuna idadi ya waumini waliosajiliwa kwa mwaka 2020 wapatao 4,518,003 kutoka katika makanisa 17,625.

Takwimu hizo zinaonesha kuwa mwaka 2020 Unioni ya Kaskazini ilikuwa na makanisa 2,406 yenye waumini 633,078 ambapo Unioni ya Kusini ilikuwa na makanisa 1,204 yenye waumini 199,320.

Katika takwimu hizo Unioni ya Rwanda ndiyo yenye idadi kubwa ya waumini wa Kanisa la Wa Adventista wa Sabato kuwa na waumini 980,593 kutoka katika makanisa 1,893 na ilikuwa na idadi ya watu 73 pekee walioliacha kanisa.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.