MTANGAZAJI

WATALAAMU WA AFYA HOUSTON WAPINGA MIKUSANYIKO

 

 Huku ikielezwa kuwa  na ongezeko kubwa la COVID-19 huko Houston,Texas  madaktari wamewataka wakaazi wa jiji hilo lenye wakaazi wapatao milioni 2.3 kujiepusha na mikusanyiko mikubwa  ya kusherehekea Mwaka Mpya.
 
 "Ninachopendekeza  watu wasifanye ni kwenda kwenye sherehe  kubwa za watu 50-60 ambapo watu wanapuliza filimbi na aina zote za mambo na kusherekea na hujui hali ya chanjo ya watu katika mazingira hayo," amesema Dk Anthony Fauci, Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa  ya Mzio na Magonjwa ya Kuambukiza.
 
 Fauci anapendekeza sherehe ndogo za familia ambao wote wamechanjwa, lakini Dk. Luis Ostrosky,Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba na Hospitali ya Memorial Hermann Hospital wamependekeza vikwako vikali zaidi.

"Samahani kusema hivi lakini pendekezo langu ni watu  kukaa nyumbani na familia zao," amesema Ostrosky huku akiongeza kuwa kuna  magonjwa mengi tu hivi  sasa na kwa kweli hakuna njia salama ya kuwa na mkusanyiko mkubwa wa bila barakoa wa  Mwaka Mpya.
 
 "Inashangaza kwamba takriban wiki mbili hadi tatu zilizopita tulikuwa na wagonjwa takribani  100 hivi katika hospitali zetu na kufikia leo tuna wagonjwa zaidi ya 580," alisema Dk. Faisal Masud, Mkurugenzi wa Matibabu wa Huduma ya Kimaadili katika Hospitali ya Methodist ya Houston.

 

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.