MTANGAZAJI

MWILI WA JASON SANTUS MTSIMBE KUSAFIRISHWA TANZANIA


Mwili wa  Kijana wa Kitanzania Jason Santus Mtsimbe mwenye umri wa miaka 24 aliyefariki ghafula huko Chattanooga Tennesse unatarajiwa kusafirishwa Ijumaa ya Disemba 31,2021 kwenda Tanzania kwa maziko yatakayofanyika kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
 
 Mama wa Jason,Dkt Mbakisya  Onyango  ambaye ni mhadhili katika Chuo Kikuu cha Tennesse ameeleza kuwa alimkuta mwanae chumbani asubuhi akiwa amefariki Dunia,ambapo usiku wa kuamkia siku hiyo waliongea na mwanaye kabla hajaenda kulala.
 
Tovuti ya Nyumba maalum za kutunza miili huko Chattanooga  ya Heritage ya www.heritagechattanooga.com imeeleza kuwa Jason aliugua kwa muda na alilazwa hospitalini mwezi Novemba 2021 na kuruhusiwa kurudi  nyumbani.

Jason alizaliwa Oktoba 11,1997 Moshi Tanzania,akapata elimu yake ya msingi jijini Arusha na Dar es salaam,Mwaka 2004 alihamia Kansas nchini Marekani yeye na Mama yake pamoja na Kaka yake Joshua Onyango ambako alijiunga na Shule ya awali ya Lee na ya  Kanisa la Waadventista wa Sabato la Manhattan,Mwaka 2010 yeye na Mama yake walihamia Chattanooga.

Akiwa Chattanooga alijiunga na Chuo Kikuu cha Tennesse na Chuo cha Waadventista wa Sabato cha Collegedale ambako alipenda Uhandisi wa Komputa,mpira wa miguu na muziki ambapo alikuwa anapiga gitaa na kuimba.


 

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.