MTANGAZAJI

TATIZO LA UTOAJI MIMBA UINGEREZA NA WALES


  

Takwimu mpya za serikali nchini  Uingereza na Wales zinaonesha kuwa robo ya mimba kwa mwaka 2019 ziliishia kwa wahusika kuzitoa.

Kwa mujibu wa mtandao wa Christian Today unaonesha kuwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (ONS) katika nchi hizo ilikusanya taarifa ya mimba 821,809 miongoni mwa wakazi nchini Uingereza na Wales kwa mwaka 2019 ambapo mimba 207,384 zilizotolewa.

 Taarifa hiyo inatanabaisha  kuwa takwimu za utoaji mimba miongoni mwa wanawake katika nchi hizo ziliongezeka kutoka asilimia 24 kwa mwaka 2018 na kufikia asilimia 25.2 kwa mwaka 2019.

Mwezi Juni,Idara ya Afya na Utunzaji wa Jamii inaonesha kuwa kulikuwa na utoaji wa mimba 209,917 miongoni mwa wanawake wanaoishi Ungereza na Wales,ikiwa ni idadi kubwa toka kutekelezwa kwa sheria ya utoaji mimba nchini humo mwaka 1968.

Msemaji wa Taasisi inayojihusisha na masuala ya Haki ya Kuishi nchini Uingereza Catherine Robinson amesema ni janga kuona kuwa robo ya ujauzito nchini Uingereza na Wales uliondolewa kwa mwaka 2019.

"Kila mmoja katika jambo hili anawakilisha kushindwa kwa jamii katika kuzuia maisha ya watoto walioko tumboni na kusaidia wanawake waliopata mimba zisizotarajiwa na huenda idadi ikawa imeongezeka kwa takwimu za mwaka 2020"Amesema Catherine.

"Kwa hiyo tunatoa wito kwa serikali ya Wales na Uingereza kukomesha tatizo la utoaji mimba"

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.