MTANGAZAJI

MAREKANI YATANGAZA LAZIMA KWA WANAJESHI KUCHANJWA


 
Idara ya ulinzi ya Marekani imesema itakuwa ni lazima kuchanjwa Chanjo ya kujikinga na Covid-19  kwa wanajeshi nchini humo kwa  kipindi cha kabla ya katikati ya mwezi Septemba mwaka huu,kwa mujibu wa Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin. 
 
Muda huo unaweza kuongezwa iwapo Mamlaka ya Chakula na Dawa itatoa uamuzi wa mwisho wa kupitisha chanjo aina ya  Pfizer,uamuzi ambao unatarajiwa kufanywa mapema mwezi ujao"Jeshi litakuwa na majuma machache ya maandalizi" amesema Austin.
 
 Mwezi uliopita kutokana na ongezeko la  kesi za  Virusi vya Covid ,Rais wa Marekani Joe Biden alisema wafanyakazi wa taasisi za Umma watahitajika kuthibitsha kuwa wamepata dozi zote za chanjo na  wale ambao bado hawajatekeleza agizo hilo wanapaswa kuvaa barakoa muda wote na kuweka umbali wa hatua sita kutoka kwa mfanyakazi mwenzake na wageni sehemu za kazi.
 
 Taarifa ya Biden ya Jumatatu imeunga mkono agizo la ulazima uliotangazwa na Waziri wa Ulinzi  Austin.
 
 "Ninajivunia kwamba wanajeshi Waume kwa Wake wataendelea kusaidia kuongeza mwamko katika vita ya janga la Corona,kama kawaida yao kwa kuonyesha mfano wa kuwalinda na kuwa salama wamarekani wenzao"Rais huyo amesema.

Kwa mujibu wa Idara ya Ulinzi ya Marekani zaidi ya wanajeshi milioni moja wamekwisha pata dozi zote za chanjo huku wengine 237,000  wakiwa wamepata dozi moja ya chanjo.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.