MTANGAZAJI

MKUTANO MKUU WA WAADVENTISTA DUNIANI WAHAMISHIWA ST LOUIS MAREKANI.

 Kamati kuu ya Utendaji  (EXCOM) ya Kanisa la Waadventista wa Sabato ulimwenguni imepitisha hivi karibuni kuhamisha eneo la kufanyia Mkutano Mkuu wa Kanisa hilo Duniani kwa mwaka 2022 kutoka Indianapolis, Indiana na kupeleka katika jiji la  St. Louis, Missouri nchini Marekani.

Uamuzi huo unafuatia taarifa ambayo haikutarajiwa kwa Uongozi wa Kanisa hilo iliyotolewa na Mamlaka ya Jiji la  Indianapolis kuwa hakutakuwa na nafasi tena ya kufanya mkutano huo Juni 6-11,2022 kama ilivyokuwa imepangwa awali.

“Wametutaarifu kuwa tarehe hizo hakuna nafasi na imekuwa ni jambo ambalo hatukulitarajia na tumetoa taarifa hii kwa kamati, tumejisikia vibaya kwa kutoendelea na uhusiano wa kufanikisha mkutano na Unioni Konferensi ya Lake,Konferensi ya Lake na Konferensi ya Indiana" amesema Ted N.C. Wilson Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Ulimwenguni.

“Hata hivyo , MUNGU alishaona tatizo na kutokana na tuliwasiliana na Uongozi wa  St Louis Convention Center, kwa tarehe ile ile ya June 6-11, 2022, tukakubaliwa . MUNGU amefungua njia"amesema

 Kamati Kuu ya Utendaji ya Kanisa la Waadventista Ulimwenguni ilishapitisha toka mwaka 2016 kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Kanisa hilo Ulimwenguni jijini St Louis kwa mwaka 2025 .

Maamuzi haya mapya yanafuatia azimio la Kamati Kuu la Januari 12 ambalo lilipitisha  kusogeza mbele Mkutano Mkuu ambao huwakutanisha wajumbe wa Kanisa hilo toka sehemu mbalimbali duniani kutoka Juni 2020 hadi Mei  20-25, 2021 kutokana na janga la  COVID-19. 

 Tovuti ya Kanisa hilo ambayo inahusu taarifa za maandalizi  ya  Mkutano Mkuu inaeleza  kuwa ni wajumbe tu  ambao watahudhuria Mkutano Mkuu wa mwakani  kama ilivyokuwa imepangwa awali tofauti na mikutano mingine ambayo hufanyika mara moja kila baada ya miaka mitano na kuwakutanisha wajumbe 70,000 na waumini wa Kanisa hilo wanaopenda kushuhudia toka nchi mbalimbali Duniani.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.