GAVANA WA TEXAS ATANGAZA WATU KUTOVAA BARAKOA
Magavana wa Majimbo ya Texas na Mississipi wametangaza kuondolewa kwa agizo la lazima ya uvaaji wa wa Barakoa katika kujikinga na Covid-19 na kuruhusu kuendelea na shughuri za maisha na mikusanyiko siku chache zijazo.
Gavana wa jimbo la Texas Greg Abbott amesema jumanne hii kuwa agizo la uvaaji wa Barakoa na vizuizi vingine vya kujikinga na Virusi vya Corona vitakoma jimboni humo Machi 10 mwaka huu ambamo ugonjwa huo umeshaua watu zaidi ya 42,000.
Hata hivyo agizo hilo limepokelewa kwa hisia tofauti na baadhi ya wakaazi,viongozi wa Texas ambao miongoni mwao wamezua mijadala kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii,Meya wa jiji la Austin lililopo Texas Steve Adler katika mahojiano na CNN amesema hakubaliani na uamuzi huo na haoni sababu ya msingi ya kufanya hivyo kwa sasa.
Huku kukiwa na kesi mpya 1,637 na vifo 59 siku ya Jumanne katika jimbo la Texas na taarifa za kesi mpya 301 na vifo 44 kwa jimbo la Mississipi.
Mara baada ya Tangazo la Gavana wa Texas,Tate Reeves Gavana wa Mississippi naye alitangaza kuondoa vizuizi vilivyowekwa kuanzia jumatano hii kuendelea na shughuli za kila siku kama kawaida.
Uamuzi wa kuondoa vizuizi hivyo unakuja saa chache baada ya tahadhari ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya usimamizi wa kuzuia magonjwa (CDC) Dkt. Rochelle Walensky ambaye alionya majimbo kutofanya uamuzi wa haraka wa kuondoa vizuizi vya kujikinga na COVID-19.
Rais wa Marekani Joe Biden amesema Marekani iko katika mkakati wa chanjo kwa watu wazima wote ifikapo mwisho mwa mwezi Mei mwaka huu ambapo kwa sasa kutakuwa na dozi moja ya chanjo tofauti na ilivyokuwa awali.
.
Post a Comment