MTANGAZAJI

FACEBOOK WAZINDUA KITABU KUTAMBUA MCHANGO WA WANAWAKE AFRIKA

Ikiwa ni maadhimisho ya Mwezi wa Kimataifa wa Wanawake Duniani,Facebook wametangaza uzinduzi wa Kitabu kiitwacho LeadHERs: Life Lessons From African Women ( 'LeadHERs:Mafunzo ya Maisha toka kwa Wanawake wa Afrika) ikiwa ni mkusanyiko wa habari za kupendeza na kuhamasisha na ushauri wa maisha ya wanawake 19 ambao wanaondoa vikwazo katika sekta za Habari,Burudani,Siasa,Elimu na Biashara barani humo.


Wanawake hao ni  akiwemo Mtanzania Vanessa Hau Mdee,Elizabeth Akua Ohene –  [Ghana]Alice Nkom -  [Cameroon],Tecla Chemabwai –  [Kenya],Baratang Miya - [Afrika Kusini],Hindou Oumarou Ibrahim - [Chad],Dkt Judy Dlamini –  [Afrika Kusini ],Hawa Sally Samai –  [Sierra Leone],Bethlehem Tilahun Alemu – [Ethiopia],Lelemba Phiri - [Zambia],Temi Giwa-Tubosun – [Nigeria],Monica Musonda – [Zambia],Saran Kaba Jones –  [Liberia],Kalista Sy – [Senegal],Yvonne Okwara – [Kenya],Tara Fela-Durotoye -[Nigeria],Noella Coursaris Musunka -[DRC],Samantha ‘MisRed’ Musa –[Zimbabwe],Djamila Ferdjani -[Niger].

 
Kitabu hicho ambacho kimezinduliwa Machi 3,mwaka huu nchini Afrika Kusini nakala zake zitapatikana bure kwa njia ya kawaida na kidijitali kina habari za maisha halisi ya kuvutia kwa ajili ya vizazi vijavyo na Viongozi vijana.Kila sura imejikita katika uzoefu walioupitia wanawake hao 19 na namna walivyokabiliana na matatizo katika kufikia mafanikio haijalishi wanatoka katika maisha,mvuto,umri ama malengo.

Waweza kupakua nakala ya  kitabu hicho hapa:LeadHERs

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.