MTANGAZAJI

ANUANI ZA MAKAZI SASA KIDIJITALI

 


Serikali ya Tanzania kupitia
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari  Dkt  Zainabu Chaula amesema kuwa wametengeneza Programu Rununu ya Anwani za Makazi na PostikodiNAPA ili kuhakikisha kuwa nchi inakuwa na mfumo wa TEHAMA wa utambuzi wa maeneo ya makazi ya watu na kukusanya taarifa ili kuwezesha utoaji wa huduma za kiuchumi na kijamii nchini Tanzania.

  Dkt. Zainab Chaula alikutana  wa wataalamu wa TEHAMA wanaotengeneza Programu Rununu ya Anwani za Makazi na Postikodi (National Addressing and Postcode Mobile Application – NAPA) mjini Morogoro ili kukagua ujenzi wa programu hiyo uliotekelezwa  na wataalamu hao.

 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara hiyo, Mhandisi Clarence Ichwekweleza amesema kuwa programu rununu ya NAPA itakuwa na faida mbali mbali ikiwemo kusajili na kuhuisha anwani za makazi,kumwezesha mtumiaji kutambua mwelekeo wa anwani kwa kutumia ramani,kutambua mitaa/vitongoji vyote vyenye anwani za makazi,kumwezesha mtumiaji kutambua mwelekeo wa anuani kwa kutumia ramani, kutambua anuani za makazi kwa kutumia namba za TIN za TRA na za NIDA,kutambua maeneo yote ya huduma za kijamii na kiuchumi kama vile benki, polisi, ofisi za Serikali,kumwezesha mtumiaji kutambua umbali wa anuani kwa kutumia ramani; kumwezesha mwananchi kupata msaada wa huduma za dharura kwa urahisi na uharaka na kuwezesha posta kuwafikia wateja wa huduma za posta kiganjani.

Akiwasilisha taarifa ya utengenezaji wa programu hiyo kwa Dkt. Chaula kwa niaba ya wataalamu wengine, Mhandisi Jampyon Mbugi wa Wizara hiyo amesema kuwa ili kufanikisha utengenezaji wa programu rununu ya NAPA wataalamu wa TEHAMA wamekusanya mahitaji ya programu hiyo, usanifu wa mfumo,uundaji wa mfumo,majaribio ya mfumo,majaribio ya kukubali kwa mfumo huo kabla ya kufanya uzinduzi wa mfumo huo ambapo kazi hiyo imeanza kufanyika  Januari 12 mwaka huu na ulitarajiwa kukamilika  Februari 28 mwaka huu ili uanze kutumika.

Naye Mhandisi Richard Magubila wa Wizara hiyo amesema kuwa programu rununu ya NAPA itaunganishwa na mifumo mingine ya TEHAMA ya Serikali kama vile ya kodi, ukusanyaji wa mapato, afya, biashara mtandao, ardhi, vitambulisho vya taifa na mifumo mingine ili kuwezesha kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi kuendana na mahitaji, mabadiliko na ukuaji wa TEHAMA nchini.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.