MTANGAZAJI

SERIKALI YA TANZANIA YASISITIZA KUFANYIA UTAFITI DAWA ZA ASILI

 

 

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi ameagiza kuwa Dawa zote za asili nchini Tanzania  ni lazima zifanyiwe utafiti kabla ya kupelekwa kwa wananchi kwa ajili ya matumizi na ili kufanikisha hilo ni lazima kuwe na rasilimali za kutoka kuwezesha kufanya tafiti za kina juu ya dawa hizo za asili.

 Profesa Makubi ametoa agizo hilo wakati wa ufunguzi kikao kazi cha viongozi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya na Vyuo vya taaluma ya Afya nchini Tanzania  kilicholenga kuboresha ushirikiano na kuangalia namna ya kuongeza rasilimali katika kuboresha tiba asili nchini kilichofanyika Dodoma ambacho pia kilihudhuriwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya nchini humo Bw. Edward Mbaga

 “Rais amekwisha toa maelekezo ya bajeti ya afya kuongezwa kwenye upande wa tiba asilia, pamoja na kuunganisha nguvu za Serikali, lakini pia taasisi bado zina uwezo wa kuchangia kuhakikisha tafiti kwa ajili ya tiba asili zinafanyika”Amefafanua Prof. Makubi

Amesema kuwa ni lazima viongozi wote wa taasisi na vyuo vya afya nchini kuwa na mtazamo chanya juu ya tiba asili kuwa zinaweza kusaidia katika kutibu magonjwa mbalimbali

“Ni muhimu kuunganisha mawazo yetu sisi viongozi na wasomi mbalimbali ili tuweze kuonyesha kwamba sisi wenyewe wasomi tunatambua mchango wa tiba asili katika nchi yetu kwa ajili ya kukinga na kutibu magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza” amesema Prof. Makubi


 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya nchini humo Bw. Edward Mbaga alikieleza kikao hicho kuwa Serikali ya Tanzania imekwisha tambua tiba asili kuwa na umuhimu toka mwaka 1969 ambapo ilielekeza Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kufanya tafiti za miti dawa ili kuweza kuleta Ushahidi wa kisayansi na kujibu maswali mbalimbali yanayohusu usalama, ubora naufanishi wa dawa za asili ambazo kwa Tanzania kuna zaidi ya miti dawa 12,000 ambayo inatibu magonjwa mbalimbali.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.