FIFA YAZINDUA MASHINDANO YA WANAFUNZI BARANI AFRIKA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) na Umoja wa Afrika wamezindua uanzishwaji wa mashindano ya mpira wa miguu kwa wanafunzi barani Afrika,makubaliano ambayo yametokana na kikao kilichofanyika Kinshasa DRC baina ya Rais wa FIFA Gianni Infantino na Rais wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC) Félix Tshisekedi, ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU).
Viongozi hao wawili ambao walianza mazungumzo siku chache zilizopita kwa njia ya mtandao kupitia video masafa walikutana ana kwa ana kwa ajili ya mazungumzo kwa lengo la kutumia nguvu ya mpira wa miguu katika kuboresha maisha na kuleta mabadiliko chanya kwa maisha ya vijana.
Wote Rais wa FIFA na Mwenyekiti wa AU kutumia muundo kazi unaotumiwa na Umoja wa Afrika,FIFA ,CAF kwa ajili ya kuendesha mashindano ya mpira wa miguu Barani Afrika ambapo mashindano hayo yataanza kufanyika DRC ambapo mkakati huo ulisainiwa katika ya FIFA na Waziri wa Michezo wa DRC.
Rais wa FIFA amesema kwa pamoja FIFA, AU, CAF na wanachama wataendeleza mashindano hayo na mafunzo ya mpira wa miguu kwa vijana kwa sababu mchezo huo ni sehemu ya maisha ya shule.
Post a Comment