MTANGAZAJI

SANAA NA MICHEZO ZILIVYOCHANGIA PATO LA TAIFA TANZANIA MWAKA 2018/2019

 

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa akiwasilisha
Muundo na Majukumu ya Wizara hiyo kwa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii January
25, 2021 jijini Dodoma.

Serikali ya Tanzania kupitia kwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa imeeleza kuwa  Sekta ya Sanaa na Michezo zimechangia katika ongezeko la pato la Taifa hilo ambapo kwa mwaka 2018, shughuli za burudani zimechangia pato la Taifa kwa asilimia 13.7 na kushika nafasi ya kwanza  na  mwaka 2019 shughuli hizo zilichangia asilimia 11.2 na kushika nafasi ya tatu.

Bashungwa alitoa taarifa hiyo wakati akiwasilisha Muundo pamoja na Majukumu ya Wizara hiyo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.

"Tunashukuru Kamati kwa kutupa mawazo chanya ambayo yatasaidia kuboresha nakuendeleza sekta hizi, naahidi mimi pamoja na timu yangu tutayafanyia kazi mawazomliyotupa na tayari tumeanza kufanya hivyo katika sekta zote"alisema Mhe.Bashungwa.

Wizara hiyo imeanza kutengeneza Mpango Mkakati wa Maendeleo ya Michezo pamoja na ujenzi wa Ukumbi wa Michezo na Sanaa (Sports and Arts Arena) ambayo itaanza kujengwa Jijini Dodoma Tanzania.

Waziri  Bashungwa ameeleza kuwa TCRA pamoja na TRA wameanza kushirikiana namna ya  kukusanya mapato ya kazi za Sanaa kupitia njia za Kidijiti (DigitalTaxation).

 Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo Stasilaus Nyongo Mbunge wa  Jimbo la Maswa Mashariki ameipongeza Wizara hiyo kwa Mikakati mizuri ya kusaidia Sekta inazozisimia, huku akishauri Wizara hiyo kuongeza ubunifu katika kukusanya mapato ya Serikali kupitia Sanaa na Michezo.   
                     

Jumanne  Sagini Mbunge wa Jimbo la Butiama ambaye ni Mjumbe wa
Kamati  ameeleza kuwa ipo haja ya kufanya mapitio ya Sera zote zilizo chini ya Wizara hiyo ili kama kuna ambazo zinahitaji marekebisho zifanyiwe maboresho ili kuendanana mahitaji ya wakati huu.



No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.