MKUTANO MKUU WA KANISA LA WAADVENTISTA ULIMWENGU (GC) WAAHIRISHWA TENA.
Kwa mara ya pili ndani ya miezi 10,Wajumbe wa Kamati Kuu ya Utendaji ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Duniani wamepitisha kuahirishwa kwa Mkutano Mkuu wa Kanisa hilo ambao awali ulikuwa ufanyike Mei 20-25 mwaka huu hadi Juni 6-11 mwaka 2022 kutokana na athari za janga la Corona duniani.
Wajumbe wa Kamati Kuu ya Utendaji toka nchi mbalimbali Duniani waliofanya kikao chao kwa njia ya mtandao wa Zoom Januari 12,2021 ambapo walipata taarifa toka kwa Viongozi wa Kanisa,Watalaamu wa Afya wa Kanisa hilo,Waratibu wa Maandalizi ya mikutano na Wanasheria na kujadili uwezekano wa kufanyika kwa Mkutano Mkuu Mei 20-25 mwaka huu huko Indianapolis,Indiana Marekani ilivyokuwa imepangwa awali na Kamati hiyo.
Kutokana na hali ya Janga la Corona ilivyo kwa sasa Duniani kwa kuzingatia masuala yanayohusu Afya,usafiri na upatikanaji wa viza za kuingia Marekani, wajumbe 185 kati ya wajumbe 194 waliopiga kura walipitisha kuupanga Mkutano Mkuu wa 61 wa Kanisa hilo kufanyika Juni 6-11,2022 jijini Indianapolis.
Tovuti ya Kanisa hilo ambayo inahusu taarifa za maandalizi ya Mkutano Mkuu inaeleza kuwa ni wajumbe tu ambao watahudhuria Mkutano Mkuu wa mwakani kama ilivyokuwa imepangwa awali tofauti na mikutano mingine ambayo hufanyika mara moja kila baada ya miaka mitano na kuwakutanisha wajumbe 70,000 na waumini wa Kanisa hilo wanaopenda kushuhudia toka nchi mbalimbali Duniani.
Post a Comment