HOSPITALI YA UHURU YAANZA KUTOA HUDUMA
Mwonekano wa sasa wa Jengo la Hospitali ya Uhuru iliyoko Dodoma ,Tanzania |
Katibu wa kuratibu shughuli za Serikali kuhamia Dodoma Meshack Bandawe akikagua vifaa mbalimbali vilivyopo katika hospitali ya Uhuru ambayo imekamilika na kuanza kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje. |
Hospitali ya Uhuru inayojengwa kwa gharama za bilioni 3.9 imeanza kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Dkt. Dkt.Eusebius Kessy ametoa taarifa hiyo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari wakati wa ukaguzi wa hospitali hiyo.
“Hospitali yetu imeanza kutoa huduma tangia tarehe 21 Desemba 2020 na mpaka sasa imeshahudumia wateja takribani 300”amesema Dkt Kessy
Ameongeza kuwa ujenzi wa hospitali hiyo ni ukombozi mkubwa kwa wananchi wa chamwino na maeneo ya karibu na kusema kuwa watahahakisha kwamba huduma zinakuwa bora kama ilivyokusudiwa
Dkt Kessy amesema kuwa hospitali iyo inatoa huduma kwa wagonjwa wenye Bima ya afya ya Taifa NHIF na Mfuko wa afya ya jamii (CHF) na pia wale ambao hawana Bima ya afya.
Akizungumzia huduma zinazotolewa kwa sasa Dkt.Kessy amesema kwa sasa huduma za maabara,clinic za macho na meno,mionzi ,clinic za mama na mtoto na huduma za wagonjwa wa nje (OPD).
Kwa upande wake Katibu wa kuratibu shughuli za Serikali kuhamia Dodoma Meshack Bandawe ambae alifanya ziara maalum kukagua imaendeleo ya Hospitali hiyo amesema kuwa kuwa ujenzi wa hospitali hiyo umekamilika kwa asilimia 99.8.
Pamoja na hayo amesema mifumo ya maji na umeme na miundombinu mbalimbali imekamilika pamoja na vifaa tiba vya Utra sound, X-ray,ECG na baadhi ya samani ambavyo vimeshawasili hospitali hapo.
Amesema siku ya sherehe za mapinduzi ya Zanzibar kulifanyika uchangiaji wa damu salama na kufanikiwa kupata unit 48 za damu.
Ujenzi wa Hospitali ya Chamwino ni agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwamba Fedha zilizotengwa kwa ajili ya sherehe ya miaka 57 ya Uhuru wa Tanzania bara za tarehe 9 Disemba 2018 zitumike kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Chamwino.
Post a Comment