JKT TANZANIA YASITISHA MAFUNZO
Jeshi la Kujenga Taifa nchini Tanzania (JKT) limesitisha kwa muda Mafunzo kwa kundi la kujitolea kwa mwaka 2020/2021 kwa vijana waliokuwa wamechaguliwa kushiriki mafunzo hayo yaliyotarajiwa kuanza hivi karibuni nchini kote.
Kaimu Mkuu wa Utawala, Kanali Hassan Mabena amewaambia waandishi wa habari kwenye mkutano wake na waandishi hao uliofanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
“Kutokana na kusitishwa kwa mafunzo hayo, JKT inawataka vijana wote ambao walichaguliwa na kuripoti makambini kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa kujitolea warejee majumbani kwao” alisisitiza Kanali Mabena.
Kanali Mabena amewataka vijana ambao waliokuwa hahawajaripoti wasiende kuripoti katika makambi waliyopangiwa mpaka watakapotangaziwa tena.
Jeshi la Kujenga Taifa limekuwa likiwajengea vijana uwezo wa kujiajiri kupitia stadi za maisha wanazopata katika mafunzo yanayotolewa kwa mujibu wa sheria na yale ya vijana kujitolea, hivyo kuwawezesha kuwa wazalendo wanaoshiriki kikamilifu katika ujenzi wa Taifa la Tanzania.
Post a Comment