MTANGAZAJI

JAMII YA KIMASAI YATAKIWA KUTUMIA UTAMADUNI WAO KUWA FURSA.

 

Katibu Mkuu Wizara ya Afya-Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt John Jingu akiwaunga mkono wajasiriamali wanawake wa kikundi cha Ereto kilichopo Kijiji cha Minjingu, Wilayani Babati kwa kununua baadhi ya bidhaa wanazozitengeneza.

 Katibu Mkuu Wizara ya Afya-Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii nchini Tanzania  Dkt. John Jingu ameitaka jamii ya kimasai nchini kutumia Utamaduni wao kama fursa ya kujiongezea kipato na  kujiimarisha kiuchumi.

 

Dkt. Jingu ameyasema hayo alipotembelea Kikundi cha wajasriamali Wanawake cha Ereto kilichopo Kijiji cha Minjingu Kata ya Nkait Wilayani Babati Mkoani Manyara kuona shughuli wanazozifanya.

 

Dkt. Jingu amesema jamii ya kimasai imezungukwa na fursa nyingi ikiwemo Utamaduni wa Jamii hiyo ambao umekuwa ukijinadi ndani na nje ya mipaka ya Tanzania

 

Hata hivyo, amesema jamii husika bado haijaitumia fursa hiyo ipasavyo kuutangaza na kuufanya kuwa chanzo cha kiuchumi ambapo akaitaka jamii hiyo  kuboresha bidhaa wanazozitengeneza kitamaduni ili ziweze kupanua wigo na soko la Kimataifa.

 

 No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.