MTANGAZAJI

BILIONI 11.04 ZATENGWA KWA AJILI YA MIKOPO YA WANAFUNZI.

 HESLB: The list of loan beneficiaries in 2019/2020 | Majina Ya Wanafunzi  Waliopata Mkopo 2019/20 | Loan application, Student loans, Higher education

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza orodha ya Awamu ya tatu yenye jumla ya wanafunzi wapya 3,544 waliopangiwa mikopo kwa mara ya kwanza katika mwaka wa masomo 2020/2021 yenye thamani ya TZS 11.04 bilioni.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari  Disemba Mosi, 2020 na
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru alisema ili kupata taarifa za kina kuhusu mikopo waliyopangiwa, wanafunzi hao 3,544 wanashauriwa kutembelea akaunti zao walizotumia kuomba mikopo kwa njia ya mtandao maarufu kama SIPA –Student’s Individual Permanent Account (SIPA).

“Kufuatia kutolewa kwa awamu hii ya tatu, hadi sasa jumla ya wanafunzi wa mwaka wakwanza waliopangiwa mikopo ni 53,364 yenye thamani ya TZS 173.29 bilioni. 

Ameeleza kuwa jumla ya wanafunzi 69,625 wanaoendelea na masomo wamepangiwa TZS 247.5 bilioni baada ya kufaulu mitihani yao ya mwaka 2019/2020.


Badru alisema baada ya kutangazwa kwa awamu ya tatu za upangaji mikopo, hatua inayofuata ni kufunguliwa kwa dirisha la rufaa kwa siku saba (07) kuanzia kesho (Jumatano, Desemba 2, 2020) ili kuwawezesha waombaji ambao hawajapangiwa mikopo au hawajaridhika na viwango walivyopangiwa kuambatisha nyaraka za ziada kuthibitisha uhitaji wao.


Kwa mujibu wa Badru alisema Katika kipindi cha rufaa, wanafunzi watahitajika
kutembelea mfumo wa olas.heslb.go.tz kufuata maelekezo na kuwasilisha rufaa zao kutoka popote walipo bila malipo yoyote  kwa HESLB” alisema Badru.

HESLB ilianzishwa na sheria mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi Julai, 2005 ili
kuwawezesha watanzania kupata elimu ya juu na kukusanya fedha za mikopo iliyoiva kutoka kwa wanufaika.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.