TUBORESHE MAKAZI KUPUNGUZA UKATILI KATIKA JAMII-DKT. JINGU
Katibu Mkuu Wizara ya Afya - Idara Kuu ya Maendelo ya Jamii nchini Tanzania Dkt. John Jingu amesema ujezi wa nyumba bora katika jamii utasaidia wananchi kuwa na makazi bora na kuondokana na vitendo vya ukatili ambavyo wakati mwingine huanzia katika ngazi ya familia.
Dkt. Jingu ameyasema hayo katka kijiji cha Ilalangulu kilichopo katika Halmshauri ya Mpwimbwe Mkoani Katavi wakati akihamasisha Kampeni ya kuboresha Makazi inayoendelea katika mikoa mbalimbali nchini.
Amesema kuwa na makazi bora ni maendeleo ya jamii kwani makazi bora yanasaidia familia kuwa na Amani na utulivu katika ustawi wao kwa ujumla.
Kwa mujibu wa takwimu za Wizaya ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto ya nchini Tanzania mwaka 2017 pekee zaidi ya matukio 40,000 ya ukatili wa kijinsi yaliripotiwa nchini humo.
Post a Comment