WADAU WAJADILI UTEKELEZAJI WA MKAKATI WA KITAIFA KUTOKOMEZA MAUAJI DHIDI YA WAZEE TANZANIA
Imeelezwa kuwa Idadi ya Mauaji ya wazee imepungua nchini Tanzania kutoka 557 kwa mwaka 2014 hadi wazee 74 mwaka 2019 na kuwa hadi mwaka huu idadi ya wanauawa kwa sababu mbalimbali ni chini ya wazee 10 mwaka mwaka.
Taarifa hiyo imetolewa jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii nchini Tanzania Sayi Magesa kwa wadau mbalimbali wanaoshughulika na masuala ya wazee nchini Tanzania waliokutana kujadili hatua iliyofikiwa ya utekelezaji wa mkakati wa Kimataifa wa Kutokomeza mauaji dhidi ya wazee
Mkutano huo unalenga kuangalia mafanikio, changamoto na malengo zaidi ya baadaye ili kufanikisha kutokomeza kabisa mauaji ya wazee.
Ripoti ya kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania ya mwaka 2009 ilionyesha kuwa wanawake wazee 2,583 walikuwa wameuawa katika mikoa minane ikiwa ni wastani wa mauaji 517 kila mwaka.
Kamishna wa Ustawi wa Jamii nchini nchini Tanzania Dkt. Naftali Ngóndi ametoa rai kwa vyombo vinavyohusika na upelelezi pamoja na hukumu kuhusu mauaji ya wazee kusaidia ili jamii itambue kuwa jambo hili ni kosa kwani wazee wana haki ya kuishi na kufurahia maisha.
Meneja wa Programu Haki kwa Wazee na ushirikiano wa Wadau kutoka Shirika la HelpAge International Joseph Mbasha amesema kwa ushirikiano na jitihada za wadau, nchi Tanzania unakwenda vizuri katika kutokomeza mauaji ya wazee kwani takwimu zimepungua sana pamoja na kuwa barani Afrika nchi nyingi zilikumbwa na janga hilo kutokana na Imani potofu.
Mmoja wa Wazee walioshiriki mkutano huo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa mashirika yanayotetea Wazee nchini Bi. Cotilda Isidory amesema tangu Serikali kupitia vyombo vyake mbalimbali iingilie kati suala la mauaji ya wazee, hivi sasa yamepungua kwa kiasi kikubwa kwani hapo kabla wameuawa wengi hali iliyokuwa inawatisha wazee hao.
Katika mkutano huo, washiriki walibainisha kuwa Serikali katika ngazi zote ikishirikiana na wadau ikiwemo vyombo vya Habari, kwa Pamoja walifanya jitihada kubwa kuhakikisha mauaji ya wazee yanakwisha.
Post a Comment