WATANZANIA WATAKIWA KUTIMIA MITANDAO YA KIJAMII KWA FAIDA.
Muongozaji wa majadiliano Bw. Michael Gwimile akifafanua jambo wakati wa mkutano wa majadiliano uliowashirikisha wadau mbalimbali wa Habari ulioandaliwa na MISA-Tan |
Watanzania wametakiwa kutoa taarifa za uhakika katika mitandao ya kijamii ili
kuondoa upotoshaji ambao umekuwa ukiongezeka kila kukicha na kuzua
taaruki kwa wananchi na serikali kwa ujumla.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika warsha ya Taasisi ya Vyombo vya Habari kusini mwa Afrika kwa hapa nchini Tanzania (MISA -TAN) iliyowakutanisha
wadau mbalimbali wa Habari kwa lengo la kuwajengea Uwezo namna ya
kuripoti Habari za COVID-19 bila kuleta taharuki katika Jamii, Msemaji Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mrakibu Msaidizi Athuman Mtasha alisema kuwa baadhi
ya watu wamekuwa wakisambaza taarifa za mamlaka mbalimbali zisizo
wahusu bila uchunguzi matokeo yake husababisha uchochezi ,takwimu za
uongo na kusababisha taharuki katika jamii hivyo ni vyema watu wakaacha
mara moja tabia ya kusambaza taarifa kwani zinaweza kuwatia hatiani.
Alisema kuwa Kwa
mujibu wa takwimu za mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kumekuwa na
ongezeko kubwa la Matumizi ya mitandao ya kijamii nchini Tanzania na ongezeko hilo limepanua wigo wa utoaji na upatikanaji wa taarifa miongoni mwa Wananchi na Taasisi mbalimbali.
Mtasha alisema
kuwa mitandao ya kijamii hususani facebook, twitter, Instagram na
youtube imewawezesha wananchi kuzalisha, kusambaza na kupata taarifa
mbalimbali za matukio yanayojiri katika jamii kwa haraka Zaidi kuliko
redio, televisheni na magazeti.
“Pamoja
na fursa hii kumekuwa na changamoto ya matumizi sahihi ya mitandao ya
kijamii zikiwemo upotoshaji, udhalilishaji na matumizi mengine yasiyofaa
na Hii inajidhihirisha kwenye kuongezeka kwa kesi za makosa ya
kimtandao katika miezi ya hivi karibuni” alisema
Afisa
sheria Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania [TCRA]Kanda ya kati Joseph
Kavishe amesema mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kwa kushirikiana na
vyombo vingine likiwemo Jeshi la polisi imeendelea kusimamia kwa ueledi
vyombo vya Habari Pamoja na watumiaji wengine wa mitandao .
Mjumbe
wa Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Michael John Gumile
ambaye pia ni Mhadhili kutoka chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohana (St.John) alisema Warsha
hiyo ya wanahabari imesaidia wadau wa Habari namna ya kuandika Habari
zitakazosaidia kuondoa taharuki katika jamii hususan katika kipindi hiki
cha Corona.
Meneja
wa kituo cha Redio,Dodoma FM ,Zania Miraji ni miongoni mwa wadau wa
Habari waliohudhuria katika warsha hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya
Vyombo vya Habari Kusini Mwa Afrika ,hapa nchini(MISA-TAN) alisema
warsha hiyo imekuwa mwarobaini wa kuwakumbusha waliojifunza kutoka
vyuoni na na maelekezo yaliyotolewa katika warsha hiyo watayafanyia kazi
hususan namna ya kuandika Habari ambazo hazina mkanganyiko pia namna ya
mwanahabari ya kujikinga
Post a Comment