MTANGAZAJI

MADEREVA 13 WAMESIMAMISHIWA LESENI ZAO KWA MUDA WA MIEZI SITA.

Kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Tanzania SACP Fotunatus Musilimu akiwa na dereva aliyekuwa anaendesha basi bila kufuata utaratibu na sheria za barabarani.
 
Madereva 13 wamesimamishiwa leseni zao kwa muda wa miezi sita na kutokujihusisha na kazi ya udereva wa magari makubwa kwa kosa la kuvunja sheria za uslama barabarani kwa kuendesha magari hayo kwa mwendo kasi.

Kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Tanzania SACP Fotunatus Musilimu ameeleza kuwa suala la ajai hapa nchini halitakiwa hata mara moja hivyo dereva yoyote atakayekiuka sheria za usalama barabarani ni lazima atachukuliwa hatua za kisheria.

Ameeleza kuwa madereva hao wote waliochukuliwa leseni zao hawaruhusiwi kujishugulisha na kzi yoyote ya udereva wa mabasi makubwa ndani ya miezi sita ila wanachoruhusiwa ni kufanya kazi za udereva katika magari madogo.

Kamishina huyo ameeleza kuwa lengo la kufungiwa kwa leseni hizo ni kudhibiti mwendokasi,kupunguza na kumaliza kabisa ajali barabarani ili kuokoa maisha ya watanzania.

Ameeleza kuwa kumekuwa na desturi ya baadhi ya madereva na wapiga debe kubashiri kwa dereva atakayewahi kufika mapema zaidi na kumpatia kiasi cha fedha kama sehemu ya pongezi na hamasa kwa madereva wengine kuendesha magari kwa mwendo kasi jambo ambalo ni hatari kwa usalama.

Wakizungumza baadhi ya makondakta na madereva wamekiri kuwepo kwa tabia ya kubert kwa baadhi ya madereva na makondakta na kulaani kitendo hicho kwani kinahatarisha usalama wa abiria na nikinyume na sheria za usalama barabarani.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.