MTANGAZAJI

WATANZANIA WENYE UWEZO WATAKIWA KUSAIDIA MAPAMBANO DHIDI YA CORONAWatanzania  wenye uwezo wametakiwa kuwa mstari wa mbele kusaidia katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Covid-19 kwa kutoa msaada mbalimbali itakayosaidia kukabiliana nao. 

Mkurugenzi wa Kiwanda cha Husseini Plastic Industries Limited cha Jijini Tanga, Yusuph Hassanali ametoa pendekezo hilo mara baada ya kukabidhi msaada wa matenki 5 yenye lita 500 kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella ikiwa ni hatua ya kuunga mkono juhudi za serikali kupambana na ugonjwa huo. 

Amesema waliamua kutoa msaada huo baada ya kupita maeneo mbalimbali kuona kuna mkusanyiko wa watu kutokana na uwepo wa ndoo zenye lita 20 hivyo alipoona hali hiyo akaona upo umuhimu wa kuweza kutoa msaada huo.

Aidha alisema kwamba iwapo wakihitaji matenki mengine wameongeza kusaidia matenki ya lita hizo huku wakiwataka wadau wengine kujitokeza kusaidia juhudi za serikali kupambana na ugonjwa huo.

Mkurugenzi huyo aliwataka wakazi wa Mkoa wa Tanga wenye uwezo wawe mstari wa mbele na sio mpaka wasubirie waombwe badala yake wahamasike kusaidia kwenye mapambano dhidi ya Corona

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.