KONGAMANO LA WANAUME WAADVENTISTA TEXAS LAFANA
Wanaume Waadventista wapatao 600 wanaotoka katika makanisa ya Konferensi ya Texas wamehudhuria Kongamano la mwaka lililopewa kauli mbiu ya UNBROKEN lengo likiwa kujifunza na kubadilisha uzoefu wa mafaniko na matatizo ya Kiroho,Jamii na Taifa wanayokumbana nayo wanaume Waadventista nchini Marekani.
Katika Hotuba yake kwenye Kongamano hilo lililofanyika ndani ya Ukumbi wa
Mikutano
wa Kanisa la Waadventista la Houston Central na kurushwa mbashara kwa
Youtube na Facebook,Mhubiri wa Kimataifa na Rais wa Amazing Facts
Mchungaji Doug Batchelor aliwataka wanaume hao kuwa na tabia ya
kusameheana katika familia,jamii na Kanisa kwa ujumla kwa kuwa kutofanya
hivyo ni kuwa mwanamme aliyevunjika katika maisha ya Kiroho na
kutokuwa na tabia ya Kristo maishani.
Akieleza
uzoefu wa Maisha yake Batchelor alisema alizaliwa kwenye familia yenye
ukwasi wa mali lakini kutokana na tabia ya Baba yake ya ulevi
ilisababisha hatimaye akajiingiza katika masuala ya ulevi,utumiaji wa
madawa ya kulevya,uhalifu na kuishi mapangoni lakini Yesu alimwita na
sasa ni mhubiri wa Kimataifa.
Rais wa US
Dream Academy,Mwimbaji wa Kimataifa na Mchungaji Wintley Phipps
aliwataka wanaume kujenga tabia ya kutotumia mabavu kwenye kila jambo
katika maisha yao ya kila siku bali wawe watu wanaokubali kusaidiwa
katika mambo ambayo hawawezi kuyatenda.
Mada
mbalimbali zilizotolewa na kujadiliwa ni masuala ya mahusiano ya wanaume
na wenza wao,matatizo ya afya na jinsi ya kukabilina nayo hasa ulaji wa
vyakula bora na mitindo ya maisha inavyosaidia kuboresha afya ya mwili
na akili huku baadhi ya wanaume wakitoa ushuhuda wa namna walivyo
nyanyaswa katika famili wakati wakiwa wadogo.
Kongamano hilo
lililohudumiwa na Waimba maarufu nchini Marekani A'Men Quartet,Neville
Peter na Mark Bunney, lililohitimishwa kwa huduma ya meza ya BWANA huku
likiwatambua wanaume wa Waadventista waliostaafu kutumikia Jeshi la
Marekani zaidi ya 20 waliohudhuria kwa kuwapa medali za kutambua mchango
wao katika jamii.
Post a Comment