MCHUNGAJI JONAS SINGO TOKA TANZANIA KUFANYA MKUTANO MAREKANI
Kanisa la Waadventista wa Sabato la New Maranatha Karibu lililoko katika jiji la Jersey Jimbo la New Jersey nchini Marekani litakuwa na Mkutano wa Uamsho kuazia Septemba 28 hadi Oktoba 12,mwaka huu.
Mkutano huo ambao utakuwa unafanyika kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 1:30 jioni kwa saa za Marekani utaendeshwa na Mchungaji Jonas Singo toka Tanzania ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Uwakili na Amana katika Konferensi ya Mashariki Kati mwa Tanzania (ECT) yenye makao yake makuu mjini Morogoro,akishrikiana na Mchungaji wa Kanisa la New Maranatha Karibu Mchungaji Moses Njuguna.
Kwaya ya New Maranatha Karibu iikiwa ni miongoni mwa Kwaya zinazoimba nyimbo za Injili kwa Lugha ya Kiswahili nchini Marekani na baadhi ya waimbaji binafsi watahudumu kwenye mkutano huo uliopewa Kauli Mbiu ya Free At Last.
Post a Comment