EMIRATES WAANZA KUHAKIKI TAARIFA ZA WASAFIRI KWA TEKNOLOJIA YA UTAMBUZI WA SURA
Shirika la Ndege la Emirates limeanza kutumia Teknolojia ya utambuzi wa sura (Facial Recognition) katika kuhakiki taarifa za wasafiri wanaotumia ndege hizo,jambo linaloelezwa kuwa litaokoa muda wakati wa ukaguzi kwenye viwanja vya Ndege.
Kupitia mtandao wa Twitter wa Emirates wameeleza kuwa shirika hilo limekuwa la kwanza kutumia huduma hiyo kwa wasafari wanaotumia Ndege zake wanaotokea Marekani na Dubai na hiyo kulifanya kuwa shirika la kwanza nje ya Marekani
kuthibitisha taarifa za mteja kwa teknolojia ya kutambua sura baada ya
Marekani kuruhusu matumizi ya teknolojia hiyo kupitia kitengo cha
udhibiti cha CBP (Customs Border Protection).
Teknolojia ya “Biometric boarding” ilitumika kwa mara kwanza kwa wateja ambao waliondoka Dubai kuelekea jiji la New York nchini
Marekani siku chache zilizopita ambapo Emirate walieleza kuwa teknolojia hiyo ilifanikiwa kutumika kwa kuwahudumia wateja kwa utambuzi wa sura kwa asilimia 100.
Post a Comment