MTANGAZAJI

HAWA NDIO WASHINDI WA WIMBO WA MKUTANO WA KIMATAIFA WA VIJANA WAADVENTISTA DUNIANI 2019 (+VIDEO)


 Tennessee Pathfinders win Oshkosh theme song contest



Roger na Ariel Lantigua ambao ni ndugu toka  Klabu ya Chama cha Watafuta Njia ya Bowman Hills  Cleveland,Tennesse ndio watunzi wa wimbo ulioshinda shindano la Wimbo Mkuu  uliotumika kwa Kambi la Kimataifa  la Watafuta Njia wa Kanisa la Waadventista wa Sabato  kutoka katika nchini 90 duniani mwaka huu.

Waratibu wa Tukio hilo walitangaza Julai  kuwa wimbo huo ulioundwa na Roger mwenye umri wa miaka 19 na Ariel mwenye miaka 18 ulikuwa umechaguliwa kuwa Wimbo Mkuu wa Kambi la Mwaka huu.

 Zaidi ya Vijana  55,000 wenye umri chini ya miaka 20 wa Chama cha Watafuta Njia pamoja na walimu wao wamehudhuria Kambi la Mwaka huu huko Oshkosh,Wisconsin kuanzia Agosti 12 hadi 17 mwaka huu tukio ambalo hufanyika mara moja kila baada ya miaka mitano.

Hadi Febrauri 2019 kulikuwa na 80 ambazo zilikuwa zimetumwa kushiriki mchakato wa kuwa wimbo wa Mkuu ambapo kila wimbo  ulipaswa kubeba ujumbe na maudhui ya kauli mbiu isemayo "Tumechaguliwa" ukibeba ujumbe wa Kristo.

Ariel na  Roger walianza kuandika wimbo huo mwaka 2014 huku wakijaribu na kukosea na ilipofika mwaka 2018 Ariel alitengeneza muziki na Roger aliandika maneno akitumia Zaburi na walifanikiwa kukamilisha wimbo huo miezi mitatu kabla ya tarehe ya mwisho ya kuwasilisha nyimbo.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.