ALICHOKIZUNGUMZA KIONGOZI WA WAADVENTISTA ULIMWENGUNI KWA MKUTANO WA VIJANA ( +VIDEO)
Mch Ted Wilson ambaye ni Kiongozi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Ulimwenguni amewataka Vijana wa Kanisa hilo kutambua kuwa wao wamechaguliwa na MUNGU kwa makusudi maalum na Kanisa linajivunia kuwa na Vijana hao,hivyo wanapaswa kumtazama Yesu Kristo na Neno la MUNGU.
Kiongozi huyo ameongoza Kanisa hilo toka mwaka 2010 alitoa agizo hilo alipohutubia zaidi ya vijana 55,000 pamoja na walimu wao walioko kwenye Kambi la Vijana Watafuta la Kimataifa toka nchi 90 duniani linalofanyika Oshkosh,Wisconsin, Marekani linalotarajiwa kuhitimishwa Agosti 17 mwaka huu.
Post a Comment