SERIKALI YA TANZANIA YAPOKEA GAWIO LA SH. BILIONI MOJA KUTOKA TPB BANK
Serikali ya Tanzania imepokea gawio la
Shilingi Bilioni Moja
kutoka Benki ya Posta Tanzania
(TPB) linalotokana na faida ya uwekezaji wake wa asilimia 83 ya hisa katika Benki hiyo katika mwaka wa fedha
2018/19.
Hafla ya makabidhiano ya Hundi
kifani ya gawio hilo imefanyika jijini Dodoma, kati ya Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) ambaye alipokea kwa niaba ya Serikali, na
Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya Benki hiyo Dkt. Edmund Mndolwa.
Akizungumza katika hafla hiyo
Dkt. Mpango aliipongeza Benki hiyo
kwa kutoa gawio kwa Serikali, na kuahidi kuwa fedha hizo zitatumika katika
shughuli mbalimbali za maendeleo nchini huku akiitaka Benki hiyo kuongeza wigo wa utoaji huduma ili kuwafikia wananchi
hususani waishio vijijini pamoja na kutoa elimu kwa wananchi hao kuhusu umuhimu
wa kuweka akiba, kukopa sambamba na kurejesha mikopo kwa wakati.
Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya TPB Dkt. Edmund
Mndolwa alisema kuwa gawio hilo ni sehemu ya faida ya Sh. Bilioni 17.2 kabla ya kodi ambayo Benki yake imeipata katika mwaka wa fedha 2018/19. Pia ameeleza kuwa Benki hiyo
itaendelea kutoa huduma bora ili kukidhi mahitaji ya wanahisa wake na wananchi
kwa ujumla.
Post a Comment