KILICHOFANYIKA SIKU YA MTANZANIA UGHAIBUNI
Picha na Habari za Freddy Macha
Siku nzima ya Mtanzania lilifana sana wiki iliyopita (Jumapili 30 Juni, 2019), London. Mafanikio ya shughuli yalitokana na ushirikiano wa vichwa vingi badala ya mtu mmoja( au wachache). Hafla ilihudhuriwa na kuhutubiwa rasmi na Balozi wetu Uingereza, Mheshimiwa Asha Rose Migiro. Wenzake karibu wote ofisini pia, walikuwepo na Juma Shah, wa kitengo cha Uhamiaji akachangia kufafanua masuala ya pasipoti mpya.
Kila mshiriki alilipa paundi 20 tu ( kama shilingi nusu laki) kiasi kinachowezekana kwa mfanyakazi yeyote Uingereza kupata chakula, vinywaji na kusikia maelezo ya wataalamu mbalimbali asubuhi hadi usiku.
Bidhaa mbalimbali za Kitanzania zilizooneshwa na Wajasiriamali
Toka kushoto. Wajasiria mali, Laila Hamza, Noeta, Anna Lukindo ( mwendeshaji wa mitindo ya "Anna Luks") na Sia Travel (Biashara ya utalii na mwalimu wa Kiswahili )
Petronella Mlewa (wa pili kutoka kushoto), anayejishughulisha sana kitaaluma na Watanzania na marafiki zao Uingereza, akiwa na baadhi ya wahudhuriaji.
Baadhi ya mavazi mengi ya Kitanzania, yaliyooneshwa
Post a Comment