MTANGAZAJI

VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA TISHIO KWA WATOTO WILAYANI PANGANI


 

Serikali wilayani Pangani imesema vitendo vya ubakaji,Ulawiti na wanafunzi kupewa ujauzito ni moja ya vitendo vya kikatili ambavyo vimekuwa tishio kwa watoto wilayani Pangani huku ikielezwa kwamba wanaofanyiwa vitendo hivyo ni kuanzia darasa la pili na kuendelea jambo ambalo ni hatari kwa ustawi wa maendeleo yao

 Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange  ametoa taarifa hiyo wakati wa Siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika kiwilaya Kata ya Pangani Mashariki iliyokwenda sambamba na uzinduzi wa Mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (Mtakuwwa) wilayani Pangani ambapo Halmashauri wa wilaya hiyo ilishirikiana na Shirika la Uzikwasa

Alisema hilo limekuwa ni tatizo kubwa sana wilayani humo huku akiitaka jamii kubadilika na kuachana na vitendo vya namna hiyo kwani vimekuwa vikikwamisha watoto kushindwa kufikia ndoto zao

Aliwataka wazazi na walezi kutoa ushirikiano wa kwenda kutoa ushahidi pindi yanapotokea matukio hayo msikubali kurubuniwa kwani kufanya hivyo tunapelekea haki kushindwa kutendeka na wahusika kuchukuliwa hatua

Naye Mwanafunzi wa shule ya Msingi Funguni Aisha Ally aliziomba mamlaka husika za kisheria kuhakikisha zinawachukulia hatua kali za kisheria watu wanaojihusisha na vitendo vya ubakaji, ulawiti na wanaowapa mimba wanafunzi kwani wanakatisa ndoto zao.

Huku wakieleza kwamba watafurahi siku moja itatokea wabakaji au wanaowalawiti wakifungwa vifungo mbalimbali kwani hivi sasa kesi ni nyingi lakini matokeo ya kesi ni madogo sana.

Siku hiyo ilikwenda sambamba na sambamba na kauli mbiu isemayo mtoto ni msingi wa Taifa endelevu tutumze, tumlinde na tumuendeleze ambapo alisema siku hizi kumekuwa na tabia ya watoto katika jamii kubakwa na kulawitiwa na watu wazima ikiwemo wengine kuwaozesha tabia ni kiyume cha sheria ya nchi.

Alisema tabia hizo zimekuwa kikwazo kikubwa cha watoto hao na wengi kushindwa kuhitimu masomo yao na kupata mimba za utotoni na kupelekea wimbi la utegemezi kwenye familia na Taifa kwa ujumla ikiwemo kuongezeka magonjwa ya zinaa na kusababnisha kupungua nguvu kubwa ya Taifa.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.