MTANGAZAJI

TANAPA YATOA TUZO KWA WADAU WA UTANGAZAJI WA UTALII NCHINI TANZANIA

Waziri wa Malisili na Utalii,Dkt Hamisi Kigwangalla akizindua  mkataba wa huduma bora kwa mteja wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa wadau mbalimbali wa Utalii ,hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha .Wengine kutoka kulia ni Kamishna Mkuu wa Uhifadhi -TANAPA ,Dkt Allan Kijazi ,Mjumbe wa Bodi -Tanapa ,Kamishna Nsato Marijani na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Arumeru ,Jerry Muro.
Waziri wa Malisili na Utalii,Dkt Hamisi Kigwangalla akizindua   Mfumo a uendeshaji wa viwango vya kimataifa (ISO 9001:2015 Quality management system) wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa wadau mbalimbali wa Utalii ,hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha .Wengine kutoka kulia ni Kamishna Mkuu wa Uhifadhi -TANAPA ,Dkt Allan Kijazi ,Mjumbe wa Bodi -Tanapa ,Kamishna Nsato Marijani na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro
Waziri wa Maliasili na Utalii ,Dkt Hamisi Kigwangalla akizungumza wakati wa utoaji tuzo kwa wadau wa utalii wakati wa hafla iliyofanyika katika hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.

Makamishna wasaidizi wa TANAPA wakifuatilia matukio mbalimbali katika hafla hiyo.
Kamishna Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Dkt Allan Kijazi akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi -Mawasiliano TANAPA,Pascal Shelutete akitangaza utaratibu wa utoaji wa tuzo hizo kwa wadau wa utalii.
Waziri wa Maliasili na Utalii ,Dkt Hamisi Kigwangalla akiwa katika picha ya pam0ja na Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group ,Joseph Kusaga ,Emilian Mallya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Jerry Muro mara baada ya kukabidhiwa tuzo ya mshindi wa tatu katika kutangaza hifadhi za taifa .
Waziri wa Maliasili na Utalii ,Dkt Hamisi Kigwangalla akikabidhi tuzo ya mshindi wa kwanza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt Ayoub Ryoba (kushoto)  wengine ni Mkuu wa wilaya ya Arumeru ,Jerry Muro (kulia).
Waziri wa Maliasili na Utalii ,Dkt Hamisi Kigwangalla akikabidhi tuzo kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Zara Adventure baada ya kuibuka mshindi wa Jumla kwa watoa huduma za Utalii katika Hifadhi za Taifa .
Waziri wa Maliasili na Utalii ,Dkt Hamisi Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mshindi wa jumla ,Zainabu Ansel ,Mkurugenzi wa Kampuni ya Zara Adventure pamoja na Kamishna Mkuu wa Uhifadhi -TANAPA ,Dkt Allan Kijazi ,Mjumbe wa Bodi -TANAPA ,Kamishna Nsato Marijani na Mkuu wa wilaya ya Arumeru ,Jeryy Muro. 
Washindi wa tuzo za Gold wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Malisili na Utalii ,Dkt Hamisi Kigwangalla.

Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)  kwa mara ya kwanza limekabidhi Tuzo kwa Wadau mbalimbali wa masuala ya Utalii  na Uhifadhi ,Tuzo zilizokabidhiwa na Waziri wa Malisili na Utalii jijini Arusha kwa lengo la kuthamini mchango mkubwa wanaotoa katika masuala ya Utalii na Uhifadhi.

Katika hafla hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Maount Meru ,Waziri Dkt Kigwangalla pia amezindua Mfumo wa uendeshaji wa viwango vya kimataifa  yaani ISO 9001:2015 Quality management System pamoja na mkataba wa huduma bora kwa mteja .

Akizungumza katika hafla hiyo iliyohudhuliwa na viongozi kutoka kampuni  na taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na masuala ya Utalii na Uhifadhi ,Mgeni rasmi ,Waziri ,Dkt Hamisi Kigwangala aliipongeza  TANAPA kwa uamuzi wa kutoa tuzo kwa wadau wa sekta ya utalii hapa nchini.

Dkt Kigwangalla alisema tuzo walizopata wadau wa sekta ya Utalii kwa kazi nzuri wanazoendelea kufanya ziwe chachu katika kuimarisha ushindani katika utoaji huduma bora katika sekta ya utalii ambapo zitasaidia kukuza uchumi wa Tanzania na akatoa wito kwa wadau wa sekta ya utalii kuwekeza katika maeneo ya usafiri na malazi kwenye maeneo ya Kusini  na Magharibi mwa mwa Tanzania.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.