WIMBO WA ROJOROJO WA NYAHANGA ULIVYOIMBWA MAREKANI (+VIDEO)
Miongoni mwa Nyimbo zilizoimbwa kwenye Tamasha la Nyimbo za Injili lililopewa jina la Sauti za Afrika Mashariki ni wimbo wa Rojorojo ulioimbwa na Whispering Hope toka Houston,Marekani.Kikundi ambacho kina waimbaji toka Kenya,Tanzania,Jamaica na Nigeria.
Whispering Hope walianza kwa kuimba wimbo wa Niambie ambao pia uliwahi kuimbwa na Kwaya ya Magomeni ya Jijini Dar es salaam Tanzania na wimbo wao wa pili ulikuwa ni Rojorojo ambao uliwafanya mamia ya watu waliohudhuria tamasha hilo kufurahi na kuimba wimbo huo kwa kushangilia.
Wimbo wa Rojorojo ni miongoni mwa nyimbo zilizoifanya kwaya ya Nyahanga iliyoko Kahama,Shinyanga Tanzania kufahamika baada ya kutoa toleo lao la tano la audio la mwaka 2012 lililopewa jina la wimbo huo lenye nyimbo 13.
Tamasha la nyimbo za Injili lililopewa jina la Sauti za Afrika Mashariki ambalo liliandaliwa na Kanisa la Nations of Praise la Houston Texas limefanyika Aprili 19-20 mwaka huu likiwahusisha waimbaji wa Umoja Central SDA Choir toka North Carolina,Whispering Hope,Morning Star,Voices Of East Africa,Tephy Achapa,Simon Morai,Allick Oswald na Mch Jules Renzano.
Post a Comment