MTANGAZAJI

WANACHANA WA EACAO WATAKIWA KUFIKIA MALENGO YA MAFANIKIO

 
Lynda Alila ambaye amekuwa mwenyekiti wa EACAO akizungumza na wanachama wa jumuia hiyo,Lynda ameshika wadhifa huo kwa muda wa miaka mitatu.



Wanachama wakimsikiliza Katibu wa EACAO Melyn Ogeto Omwega akitoa taarifa yake.
Viongozi na wanachama wa Jumuia inayowaunganisha  Waadventista toka Afrika Mashariki waishio Houston Marekani (EACAO) wametakiwa kuhakikisha wanashrikiana  kuweka malengo ambayo yataleta manufaa kwa wanachana wa umoja huo walioko Marekani na kuleta chachu ya maendeleo katika nchi wanazotoka.

Katika Kikao cha Kwanza cha mwaka 2019 ambacho kilihudhuriwa na viongozi na baadhi ya wanachama kilichofanyika hivi karibuni ambapo Mchungaji Philemoni Mswanyama ambaye alianzisha wazo la kuwa na jumuia hiyo mwaka 2014 akaeleza kile wanachopaswa kukifanya viongoni na wanachama wa  EACAO

                                    
Jumuia ya Waadventista wanaotoka  katika nchi za Afrika Mashariki waishio Houston (EACAO) ilianzishwa rasmi Mei 2016 kwa lengo la kusaidia wanachana wanaopatwa na matatizo hasa wakati misiba kwa sasa inawachama hai 94 ikiwa imeshawezesha kupatikana kwa misaada ya  matukio 11 ya misiba yaliyowapata wanachama.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.