MKUU WA WILAYA AWATAKA WANAWAUME KUWAPA WANAWAKE HAKI YA KUMILIKI ARDHI
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa na viongozi mbalimbali akiwa kwenye banda la mradi
wa urasimishaji ardhi vijiji (LTA) ambao ndio wamesaidia kutoa hati
miliki kwa wanawake na kupunguza migogoro wilaya ya Iringa
|
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amewataka wanaume kuwapa haki wanawake ya kumiliki ardhi kwa kuwa wanahaki
hiyo kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi hivyo mwanaume
atakayemkataza mwanamke kumiliki ardhi atachukuliwa hatua za kisheria.
Akizungumza
kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Iringa Richard Kasesela katika kilele cha
maadhimisho ya wanawake yaliyofanyika katika kijiji cha Ibangamoyo kata
ya Ulanda wilaya ya Iringa alisema kuwa wanawake waaze kumiliki ardhi
ili kujiinua kiuchumi kwa kuwa wanawake ndio walezi wa familia tofauti
na wanaume wanaokuwa na makazi tofauti tofauti.
Amesisitiza kuwa Wanawake mkoani humo wanapaswa kumiliki ardhi kwa ajili ya kufanya
shughuli za kimaendeleo na badala yake waachane na tamaduni kandamizi za
kuwaachia wanaume katika umiliki wa mali.
Post a Comment