IKULU YA MAREKANI ILIVYOMKABIDHI ANNA HENGA MKURUGENZI WA LHRC TANZANIA TUZO YA UJASIRI (+VIDEO)
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Bi. Anna Henga amekuwa miongoni mwa wanawake 10 waliotunukiwa Tuzo ya Mwanamke Jasiri (mwenye uthubutu) Duniani (International Women of Courage Award), 2019, tuzo inayoandaliwa na Ikulu ya Marekani chini ya Katibu Mkuu Kiongozi, Mike Pompeo ambaye ndiye aliyekabidhi tuzo hiyo akiwa na Mke wa Rais wa Marekani Melania Trump.
Tuzo hiyo ilitolewa Machi 7,mwaka huu katika Ikulu ya Marekani na tukio hilo lilioneshwa mbashara kupitia twitter,Facebook na Tovuti ya Ikulu ya Marekani
Bi. Anna Henga alitajwa kuwa ni moja ya wanawake waliotunukiwa tuzo hiyo kufuatia juhudi zake katika utetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania hasa kwa upande wa jamii ya kimaasai.
Wanawake wengine tisa waliotunukiwa tuzo hiyo wanatoka katika nchi za Egypt, Jordan, Ireland,Bangladesh, Burma, Djibouti,Montenegro, Peru na Sri Lanka.
D.C. Anna Henga anakuwa ni Mtanzania wa pili kutunukiwa Tuzo ya Kimataifa ya Mwanamke Jasiri, akifuata nyayo za Vicky Ntetema aliyepata tuzo hii mwaka 2016
Tuzo ya International Women of Courage ilianzishwa mwaka 2007 ili kutambua mchango wa wanawake wanaojitoa kwa nguvu na ujasiri kama viongozi katika kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii zao bila kujali hatari ya maisha yao binafsi.
Mpaka sasa, kupitia tuzo hiyo Ikulu ya Marekani imetambua mchango wa wanawake zaidi ya 120 kutoka nchi zaidi ya 65 katika kutetea haki za binadamu, kudumisha nafasi ya wanawake katika jamii, amani na utawala bora katika nchi zao.
Post a Comment