TASWIRA YA FLYOVER YA TAZARA BAADA YA MAGARI KURUHUSIWA KUPITA
Muonekano wa njia ya juu (flyover) katika makutano ya barabara za Nyerere na Mandela eneo la TAZARA jijini Dar es salaam baada ya magari kuruhusiwa kupita juu yake.
Kufunguliwa kwa flyover hizo kunaelezwa kuwa kumepunguza
adha ya foleni safari kutoka
katikati ya jiji hadi uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere
hivi sasa huchukua si zaidi ya nusu saa badala ya masaa mawili au matatu
ya awali. Picha na Muhidin Issa Michuzi
Post a Comment