Nchini
zilizopiga hatua katika maendeleo ya Sayansi na Teknolojia zimetakiwa
kuwa tayari kusaidia kuleta teknolojia hiyo ili kukabiliana na athari
zinazoweza kujitokeza za kimazingira katika harakati za kufikia
maendeleo ya uchumi wa viwanda.
Akizungumza
kwenye maadhimisho ya 72 ya Umoja wa Mataifa (UN) na wageni waalikwa
kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais, Samia
Suluhu Hassani amesema kwamba maendeleo ya viwanda yanakwenda sambamba
na tishio la uharibifu wa mazingira na tabianchini ni muhimu kwa wadau
wote wa maendeleo kujipanga.
Amesema
nchini juhudi zinaendelea za kukuza uchumi na maendeleo ya watu lakini
ni muhimu kwa wananchi kwa ujumla wao kuweza kulinda na kuhifadhi zaidi
maliasili, hifadhi na rasilimali za taifa ili kuweza kufikia uchumi wa
viwanda.
- Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan
akisalimiana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro
Rodriguez mara baada ya kuwasili kwenye maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja
wa Mataifa yaliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es
Salaam.
Aliongeza
kwamba ofisi yake ambayo inashughulikia mambo ya tabianchini na
mazingira wametunga sera, sheria na sera mpya ya mazingira na uendeshaji
wa mambo ya mazingira pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2016 ambapo
ni kuhakikisha juhudi za viwanda haziwezi kuathiri mazingira ya nchini
Amesema
kwamba ni takribani miaka miwili tangu kuanzishwa kwa agenda za
maendeleo endelevu 2030, ambapo malengo 17 yamewekwa na Tanzania
imefanikiwa kuingia kwenye awamu ya pili ya maendeleo endelevu katika
juhudi za kupambana na umasikini
- Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan
akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki na
Afisa Mwakilishi wa Unesco Dar, Ann Therese Ndong- Jatta mara baada ya
kuwasili katika viwanja vya Karimjee kushiriki maadhimisho ya miaka 72
ya Umoja wa Mataifa.
- Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan
akisalimiana na Mwakilishi wa UNFPA nchini, Jacqueline Mahon mara baada
ya kuwasili katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
- Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan
akisalimiana na Mwakilishi wa UNICEF nchini, Maniza Zaman mara baada ya
kuwasili katika maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja wa Mataifa
yaliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
sss
- Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan
akipokea heshima katika maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja wa Mataifa
yaliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
- Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan
akikagua gwaride la heshima katika maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja wa
Mataifa yaliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
- Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan,
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Kikanda na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk.
Augustine Mahiga pamoja na 10) Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa
(UNDP), Alvaro Rodriguez wakishuhudia bendera ya Umoja wa Mataifa
ikipandishwa kuashiria kilele cha maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja huo.
- Waziri
wa Mambo ya Nchi za Nje, Kikanda na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk.
Augustine Mahiga akiazungumza machache kabla ya kumkaribisha Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan (hayupo
pichani) kuzungumza kwenye maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja wa Mataifa
yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
- Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan
akihutubia hadhara ya wageni mbalimbali (hawapo pichani) na kusisitiza
umuhimu wa teknolojia katika kufikia uchumi wa viwanda wakati wa
maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye viwanja
vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
- Picha
juu na chini ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro
Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa Mataifa kwenye maadhimisho ya miaka
72 ya Umoja wa huo yaliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar
es Salaam
- Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akimkabidhi tuzo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu
Hassan ya heshima kwa kutambua ushirikiano wa Tanzania katika Umoja wa
Mataifa wakati wa maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja huo.
- Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akimkabidhi tuzo
ya heshima Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Kikanda na Ushirikiano wa
Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga wakati wa maadhimisho ya miaka 72 ya
Umoja huo.
- Pichani
juu na chini ni baadhi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, viongozi wa
Serikali pamoja na wadau wa maendeleo waliohudhuria sherehe za miaka 72
ya Umoja wa Mataifa.
- Wanafunzi wa shule ya sekondari Weruweru wakitoa burudani kwa vitendo kwenye maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja huo.
- Mgeni
rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia
Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na wakuu wa mashirika yaliyochini
ya Umoja wa Mataifa nchini wakati wa maadhimisho ya miaka 72 ya Umoja
huo.
- Mgeni
rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia
Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na mabalozi wanaoziwakilisha nchi
zao Tanzania
- Mgeni
rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia
Suluhu Hassan katika picha ya pamoja wanafunzi wa shule ya Sekondari
Dodoma, Weruweru na Zanzibar.
- Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje katika picha ya pamoja.
- Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akiagana na
baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za miaka 72 ya Umoja wa
Mataifa yaliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Post a Comment