MTANGAZAJI

MWIMBAJI WA THE LIVING VOICES YA UGANDA AFARIKI BAADA YA KUGONGWA NA GARI Mwimbaji Mahiri wa Sauti ya Tatu na mmoja wa Walimu wa  kwaya ya Nyimbo za Injili The Living Voices ya Kanisa la Waadventista Wa  nchini Uganda Nyombi  Steven amefariki dunia jana usiku baada ya kugongwa na gari wakati akielekea nyumbani baada ya kutoka Kazini.

Akizungumza na mtandao huu  Kutoka Kampala Uganda hii leo Mwalimu wa The Living Voices  Enock Kaawaase ameelezea kuwa  kifo cha Marehemu Nyombi kilitokea jana usiku baada ya kugongwa na gari ambalo lilikuwa halikuwasha taa na kisha kupoteza maisha papo hapo na  mipango ya mazishi inafanyika kijijini kwao na Marehemu ambapo mwili wake ulitarajiwa kusafirishwa hii leo kutoka Kampala.

Marehemu Nyombi aliyezaliwa miaka 45 iliyopita  alikuwa ni Miongoni mwa waimbaji waanzilishi wa The Living Voices ambayo nyimbo zao husikika kupitia Morning Star Radio na Morning Star TV alimpoteza mama yake akiwa na miaka 11 na kulelewa na Shangazi yake ambaye ni mwimbaji na analala mauti akiwa amedumu katika kwaya hiyo kwa muda wa miaka 16.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.