MTANGAZAJI

WAIMBAJI WA THE LIGHT BEARERS WALIPOKUTANA NA BILL GAITHER KATIKA STUDIO ZAKE

 Waimbaji wa The Light Bearers toka Dar es salaam Tanzania leo Septemba 25,mwaka huu wamepata nafasi ya kutembelea katika studio za waimbaji wa Gaither zilizoko Alexandria nchini Marekani ambapo walipata nafasi ya kuimba nyimbo 6 katika studio hizo na kufanya mazungumzo na Bill Gaither pamoja na  mkewe.

Baada ya kutoka hapo waimbaji hao ambao wako nchini Marekani kwa siku 45 wameelekea katika kanisa la Waadventista Wa Sabato la Umoja lililoko Raleigh,North Carolina nchini Marekani ambako watashiriki katika juma la Uamsho linaloanza leo ambapo mhutubu atakuwa ni Mchungaji Baraka Butoke toka Tanzania.No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.