MTANGAZAJI

CHATO:BENKI YA CRDB YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA


Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja mwaka huu 2017, benki ya CRDB jana simetoa semina kwa wateja wake katika wilaya ya Chato mkoani Geita na pia kupokea maoni yao ili kuboresha zaidi huduma zake.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wakubwa Goodlack Nkini aliwahakikishia wateja wa benki hiyo huduma ya mikopo kwa muda wa siku saba na hivyo kuwahimiza wafanyabiashara kuitumia benki fursa hiyo kukuza mitaji yao ya biashara.

Aidha alisisitiza kwamba benki hiyo itaendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake ikiwa ni benki inayoongoza kwa kutoa mikopo hapa nchini huku pia jamii ikiendelea kunufaika na benki hiyo kupitia gawio la faida ambalo hutolewa kila mwaka ili kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo afya na elimu.

Meneja wa CRDB tawi la Chato, Msigwa Mganga alisema benki hiyo imeendelea kuwafikia wateja wake kote nchini kupitia huduma mbalimbali ikiwemo Fahari Huduma, Simu Banking pamoja na Internet Banking na hivyo kuwa benki yenye mtandao mkubwa unaowawezesha wateja wake kupata huduma za kibenki popote walipo.

Baadhi ya wateja wa CRDB, Mellia Alloyce pamoja na Ristides Ramadhan walikiri kunufaika na benki hiyo kupitia huduma mbalimbali ikiwemo huduma ya mikopo na hivyo kukuza biashara zao huku hivi sasa wakifurahia uharaka wa huduma hiyo tofauti na hapo awali.
Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wakubwa Goodlack Nkini, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji CRDB. Meneja wa CRDB tawi la Mwanza, Wambura Calystus akizungumza kwenye semina hiyo. Meneja wa CRDB tawi la Chato, Msigwa Mganga akizungumza kwenye semina hiyo. 
        Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Chato, Mwl.Delphina Cosmas , akichangia mada kwenye semina hiyo.        

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.