WAZIRI WA FEDHA WA TANZANIA AKAGUA NA KUTOA MAAGIZO KUHUSU MADINI YA ALMASI YALIYOKAMATWA
Sehemu ya Mzigo wa Almasi uliokamatwa katika uwanja wa Ndege ambao thamani yake ni zaidi
ya Tsh. Bilioni 64.
|
Waziri wa Fedha na
Mipango Dkt. Filip Mpango akisoma maelezo ya mzigo huo ambayo yalikuwa tofauti
kabisa na uhalisia mara baada ya kuhakikiwa na timu ya Wataalamu wa Kitanzania wazalendo.
|
Waziri
wa Fedha na Mipango nchini Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango ameviagiza vyombo
vinavyohusika kuchukua hatua za kisheria dhidi ya kampuni ya Williamson Diamond
Ltd na wote waliohusika kuidhinisha usafirishaji wa madini ya almasi kutoka
migodi ya kampuni hiyo na kudanganya thamani halisi ya madini hayo kwa lengo la
kuisababishia hasara Serikali.
Dkt.
Mpango ametoa agizo hilo leo septemba 09 baada ya kukagua madini ya almasi
yaliyokamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es
Salaam yakisafirishwa kupelekwa nchini Ubelgiji.
Miongoni
mwa hatua za kisheria zitakazo chukuliwa na serikali ya Tanzania ni pamoja na
kutaifisha madini yote ya almasi yaliyokamatwa baada ya kubainika udanganyifu
wa thamani yake halisi.
Almasi
hiyo ilikamatwa Agosti 31 mwaka huu muda mfupi kabla ya kupakizwa kwenye ndege
ili isafirishwe kwenda nchini Ubelgiji, na ilipochunguzwa ilibainika kuwa
nyaraka za kampuni ya Williamson Diamond Ltd zimeonesha kuwa almasi hiyo ina
thamani ya Dola za Marekani Milioni 14.798 sawa na Shilingi Bilioni 33 za
Tanzania wakati thamani yake halisi ni Dola za Marekani Milioni 29.5 sawa na
Shilingi Bilioni 65 za Tanzania.
Post a Comment