MTANGAZAJI

THE LIGHT BEARERS TOKA TANZANIA WAREKODI NYIMBO 10 KATIKA KITUO CHA TELEVISHENI CHA CCX MAREKANI








Waimbaji wa The Light Bearers (Pichani) toka Dar es salaam,Tanzania leo wamepata nafasi ya kurekodi nyimbo zao  katika kituo cha Televisheni cha CCX Community TV kilichopo Minneapolis,Minessota nchini Marekani ambako wako huko kwa ziara ya siku 45 wakihudumu kwenye mikutano mbalimbali ya njili nchini humo.

Wakati mtandao huu ukizungumza na Kiongozi wa Waimbaji hao Waziri Barnabas amesema walikuwa wanaendelea na zoezi hilo na tayari walikuwa wamesharekodi nyimbo saba ambazo pamoja na zingine tatu na kufanya idadi ya nyimbo 10 ambazo  zitakuwa zikirushwa na kituo hicho ambacho pia hutangaza baadhi ya vipindi vyake kwa Lugha ya kiswahili kwa ajili ya Afrika,Marekani na maeneo mengine wanaozungumza kiswahili.

Wakiwa katika kituo hicho cha Televisheni walipokelewa  na Ndugu Mike ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa CCX Community TV 

The Light Bearers watakuwa mjini Minneapolis kwa majuma matatu wakiendelea kutoa huduma ya uimbaji kwenye Kanisa la Mount Of Blessings la Waadventista Wa Sabato baada ya hapo wataelekea Raleigh,NC kwa juma la Uamsho na kisha wataendelea na ziara yao katika maeneo mengine huko New Jersey na Texas kukamilisha siku 45 nchini humo.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.