MTANGAZAJI

VIDEO:UTAKACHO KISHUHUDIA KATIKA SANTURI MWONEKANO NAMBA 3 YA THE LIGHT BEARERS

 

Mwishoni mwa mwaka 2016 waimbaji wa The Light Bearers toka Tanzania  walisafiri kwenda mjini Reading,Uingereza kwa ajili ya kutoa huduma ya nyimbo katika mkutano wa Injili nchini humo.

Waimbaji hao walitumia fursa hiyo kurekodi video za nyimbo ambazo zitakuwa katika Santuri mwonekano namba tatu iitwayo Mzabibu wa kweli ambayo imetayarishwa na kuongozwa na Tegemea Champanda mtayarishaji wa Audio Visual Studio.

Miongoni mwa Nyimbo zinazotarajiwa kuwemo katika toleo hilo ni Mungu Kimbilio ambao mtararishaji na Mwongozaji amejaribu kuonesha maeneo mbalimbali ya Uingereza ambayo waimbaji wa The Light Bearers waliyatembelea na kutoa huduma mbalimbali za Uimbaji nchini Uingereza.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.