MTANGAZAJI

DAR ES SALAAM:MKUTANO WA TMI MWENGE WASHIKA KASI

Waongozaji wa Mkutano Peace Munisi na Samweli Philipo

Kwaya ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato Ukonga



Kwaya ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato Mikocheni A


Mch Aston Mmamba

Dr Lucas Rugemalila Nzungu




Mkutano wa TMI unaorushwa mubashara na Vyombo vya Habari vya Kanisa la Waadventista Wa Sabato nchini Tanzania (Morning Star Radio na Televisheni) kwa njia ya satalaiti na mitandao ya kijamii ambao unashuhudiwa na  watu kutoka  nchi mbalimbali duniani unaendelea katika kanisa la Mwenge kila siku kwa majuma matatu kuanzia saa 11:30 jioni hadi saa 2:00.

Mkutano huo ambao pia unaambatana na matendo ya huruma kwa jamii nchini Tanzania yanayofanywa na waumini wa kanisa hilo unaangazia masuala ya Afya,Kaya na Familia na Neno la Mungu bila kusahau waimbaji toka katika kwaya 66 za jijini Dar es salaam,Pwani na Morogoro.

Katika hotuba zinazoendelea kutolewa  Dr Josia Tayali alilisitiza jamii kuzingatia kanuni bora za afya ili kuwa na afya bora kwa kila mtu ikiwemo ulaji mzuri,kufanya mazoezi yanayofaa,kulala mapema na kwa muda unaotakiwa ,huku Mch Aston Mmamba ambaye alizungumzia suala la mawasilino kwa wanandoa na hasa suala la kusikilizana katika mawasiliano.

Naye Dkt Lucas Rugemalila Nzungu alisisitiza kujikita katika utumiaji wa akili katika kujifunza na neno la MUNGU na kufahamu mafundisho ya kweli na si kufuata nadharia za watu binafsi wanaojiita kuwa ni watu wa MUNGU huku wakiwa kinyume na mafundisho hayo.

Mpaka sasa kwaya zilizokwisha toa huduma ya uimbaji  kwenye mkutano huo unatarajiwa kumalizika Julai mosi ni 10.
Waweza kupata matangazo ya mubashara toka Mwenge kwa njia ya Satalaiti kwa kufuata maelekezo haya yanayorushwa kutokea kanisa la Mwenge Dar es salaam. Satellite ni ABS 2
Frequency 11629
Symbol Rate 3749
Polarization V
Bila kutumia king'amuzi cha kulipia
Kuanzia saa 11:30 jioni #TMITANZANIA17

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.