MTANGAZAJI

DAR ES SALAAM:KWAYA 66 KUIMBA MUBASHARA KWENYE MKUTANO JIJINI



Jumla ya kwaya 66 zitashiriki kutoa huduma ya nyimbo kwenye mkutano wa Setallite utakao rushwa mubashara kupitia Morning Star Radio na Morning Star Televisheni wa majuma matatu toka Kanisa la Waadventista Wa Sabato Mwenge kuanzia Juni 10 mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa hivi karibuni na Mkurugenzi wa Muziki wa Kikristo katika Jimbo Kuu la Kusini mwa Tanzania Mchungaji Joseph Dzombe inaeleza kuwa kwaya hizo ni kutoka katika makanisa mahalia ya Jimbo la Kusini Mashariki (SEC) na Mashariki na Kati mwa Tanzania (ECT) zilizoko katika mikoa ya Dar es salaa,Pwani na Morogoro.


Morning Star Radio imeshuhudia viongozi wa kwaya hizo wakipewa maelekezo ya jinsi ya kushiriki katika mkutano huo na Kamati inayoratibu uimbaji ambapo ratiba ya awali inaonesha kuwa kila siku kutakuwa na kwaya si chini ya tatu zitakazohudumu huku mkutano huo ukitaraji kuanza kila siku saa 12 jioni hadi saa 2:00 usiku.


Kanisa la Waadventista Wa Sabato Mwenge litakuwa ni kituo kikuu cha mikutano ya TMI inayotarajiwa kuwahusisha waumini wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato nchini Tanzania.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.