MTANGAZAJI

KUNDI LA ACAPPELLA TOKA GOMA,DRC

Aina ya Uimbaji wa Muziki wa Injili wa Acappella katika Kanisa la Waadventista Wa Sabato ni uimbaji unaoelezwa kuwa ni mkongwe na unapendwa na waumini wengi wa kanisa hilo duniani.

Katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati asilimia kubwa ya wapenzi wa aina ya muziki wa Acappella ni vijana huku ikielezwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi katika ukanda huo ambapo vijana wanashiriki kuimba aina hii ya uimbaji.

Huko DRC nako kuna makundi yanayoimba aina hii ingawa nchi hiyo inasifika kwa kuwa na waimbaji wengi wanaopenda kutumia ala za muziki zaidi.
Acappella ni aina ya uimbaji ambao hautumi ala za muziki na hivyo huhitaji umahili wa kutengeneza nyimbo zenye muafaka kwa mwimbaji binafsi akiwa anaimba katika kundi ama kwaya.

Il est Écrit ni kundi la Uimbaji wa Acappella katika Kanisa la Waadventista Wa Sabato mjini Goma,DRC wakiwa tayali na toleo moja la Audio hapa tumekuwekea video yao

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.