MTANGAZAJI

THE LIGHT BEARERS WAIMBAJI TOKA TANZANIA WASHIRIKI TAMASHA LA AMBASSADORS OF CHRIST MJINI KIGALI,RWANDA


Waimbaji wa Kike wa The Light Bearers wakiwa tayali kwa shooting video mjini Kigali leo Desemba 25Desemba 20,2016 waimbaji wa The Light Bearers toka jijini Dar es salaam,Tanzania walisafiri kuelekea Kigali,Rwanda kwa ajili ya kushiriki kwenye tamasha la kimataifa la kutimiza miaka 20 ya waimbaji wa Ambassadors of Christ ya jijini humo.

Desemba 24,2016 ndipo ilikuwa siku ya tamasha lenyewe ambapo walipata nafasi ya kuimba jukwaa moja na Ambassadors of Christ kwa mara ya kwanza toka LB waanze kuimba miaka takribani mitatu uliyopita,katika tamasha hilo ambalo linaelezwa kuhudhuriwa na watu takribani 7,000 walifanikiwa kuimba nyimbo nne pamoja na waimbaji mbalimbali walioarikwa huku asubuhi yake wakipata nafasi ya kutoa huduma ya uimbaji kwenye Kanisa la Waadventista Wa Sabato Remera ambalo linaelezwa kuwa na kwaya 25 na lile la Kigali Linaloendesha Ibada kwa Lugha ya Kiingereza

Viongozi waandamizi wa The Light Bearers Waziri Barnabas na Dr Peter Mabula na Mwalimu Fredy Kirya wakizungumza na mtandao huu toka Kigali hii leo wamesema safari yao ya Rwanda imewapafunzo kubwa la namna ya kuboresha uimbaji hapa nchini na hasa kuona namna wanyarwanda wanavyopenda muziki wa injili kutokana na kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo.

Wakiwa mjini Kigali  leo waimbaji hao wameendelea kufanya shooting ya video yao nyingine ambayo inarekodiwa na Msanii Records kwa ushirikiano na JCB Studioz.

1 comment

Unknown said...

Good move Light Bearers.

Vema sana kwa hatua hiyo kubwa..Mungu atawajaza baraka na mtafanya mambo makubwa katika uinjilisti.

Tunataraji kuwaona Musoma... "Msanii Records"

By Agape Gospel - Musoma TZ

Mtazamo News . Powered by Blogger.