MTANGAZAJI

DAR ES SALAAM:MADEREVA 10 WA TANZANIA WALIOTEKWA NCHINI CONGO WAREJEA NCHINI NA KUSEMA WALIPONEA TUNDU LA SINDANO KUUAWA


 Madereva hao wakipokelewa uwanjani hapo.
 Madereva hao wakiwa chumba cha mkutano cha uwanja huo wakati wa mapokezi yao.
Dereva  Mbwana Said (kulia), akielezea jinsi walivyotekwa.
 Dereva Kumbuka Seleman (kulia), akisimulia jinsi alivyotoroka na kutoa taarifa ya kutekwa kwao.
Dereva  Athuman Fadhili (kulia), akisimulia walivyookolewa na majeshi ya Congo na jinsi walivyojificha porini na kutembea umbali mrefu kwa kutambaa ambapo ilifika wakati waliomba bora wafe kuliko mateso waliyokuwa wakipata.
 Hapa ni furaha ya kukutana na ndugu jamaa na wafanyakazi wenzao.
 Picha ya pamoja na viongozi waliowapokea.
 Ndugu, Jamaa, marafiki na wafanyakazi wenzao wakiwa nje ya jengo la VIP uwanjani hapo wakisubiri kuwapokea.


Hapa Dereva Mbwana Said akikumbatia na mjomba wake Kassim Salim katika hafla hiyo kwa Mbwana ilikuwa ni furaha na majonzi. 
Mbwana Said (katikati), haamini macho yake baada ya kukutana na mke wake Mariam pamoja na mtoto wake Kauzari.

Madereva 10 wa Tanzania waliotekwa na watu  wanaodhaniwa ni waasi Jamhuri ya Demokraia ya Congo (DRC) wamesema waliponea tundu la sindano kuuawa.

Kauli hiyo imetolewa na madereva hao katika hafla ya kuwapokelewa iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam jana jioni.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake Mbwana Said alisema analishukuru jeshi la Congo kwa jitihada kubwa walioifanya kwa ajili ya kuokoa maisha yao." 

Alisema walilazimia kutembea kwa muda mrefu huku risasi zikirindima kati ya majeshi ya serikali na waasi hao hadi walipofanikiwa kutuokowa kutoka kwenye mikono ya waasi hao. 

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Suzan Kolimba aliishukuru serikali ya Congo kwa jitihada iliyoifanya na kufanikiwa kuwaokoa madereva hao.

Balozi wa Congo nchini Jean Mutamba aliwataka madereva hao kuacha viza na nyaraka zao ubalozini pindi wanapo safiri na kurudi ili iwe rahisi kuwatambua pale wanapopata matatizo.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.