MTANGAZAJI

MWANZA:SERIKALI YALIPONGEZA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO JIJINI MWANZA


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali za watu binafsi zikiwemo zile za kidini na kijamii katika kufanikisha maendeleo ambapo amelipongeza Kanisa la Waadventista wa Sabato la Ilemela Jijini Mwanza kwa hatua yake kujenga Hospitali ya Kisasa ambayo itakuwa msaada katika Wilaya hiyo.

Dk. Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za miaka 50 ya Jubilee ya kuanzishwa Utume wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato katika jiji la Mwanza tukio lililofanyika siku ya Julai 3.2016 kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

Akitoa hotuba za kufunga sherehe hizo, Dk. Kigwangalla amelipongeza kanisa la Kirumba kuwa na jubilee ya miaka 50 Lakini pia amelipongeza kwa huduma ya malezi ya vijana wa kanisa hilo wakingali wadogo na kwamba kwa kufanya hivo ni kuliandaa kanisa na Taifa kwa ujumla kuwa na viongozi waadilifu.

Dk. Kigwangalla ameyataka madhehebu ya dini yawe mstari wa mbele katika kukemea maovu ili Taifa lidumu kuwa na Amani.


Aidha, katika hutuba hiyo, Dk. Kigwangalla aliwahakikishia uongozi wa kanisa hilo kuwa Hospitali yao mpya inayojengwa Serikali itakuwa nao bega kwa bega na kuaahidi kutoa ushirikiano katika suala hilo la ujenzi pamoja na uendeshaji wa Hospitali hiyo kwa lengo la kuboresha afya za Wananchi wote.

Katika hatua nyingine, Dk. Kigwangalla alikemea vitendo vilivyoanza kushamili ikiwemo baadhi ya watu kushabikia masuala ya mapenzi ya jinsia moja ambapo ikiwemo suala la ushoga.


Aidha, katika tukio hilo, Dk. Kigwangalla alipata kutembelea ujenzi wa Hospitali hiyo mpya na ya kisasa inayotarajiwa kukamilika kwake hapo baadae na kisha kuwasili kwenye viwanja vya CCM Kirumba ambapo pia alipata kukagua gwaride la vijana wadogo, wa kati na wa kanisa hilo ambao ni pamoja na vijana waliopatiwa mafunzo ya Kiroho, Kimwili na Kikakamavu wakiwemo Wavumbuzi (adventure) Watafuta njia (path finder-Pf), Mabalozi na Kiongozi Mkuu (Master Guide)
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati mwenye suti ya bluu) akiwa katika jengo la kisasa linalojengwa kwa ajili ya Hospitali ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Jijini Mwanza.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa maelezo namna ya miundo ya Hospitali na viwango vyake..
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kanisa hilo
Kituo cha Afya kilichopo kwa sasa kikiendelea na huduma
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakitoka walipotembelea jengo hilo la Hospitali linalojengwa..
Picha ya jengo hilo la Hospitali pindi litakapokamilikaMuonekano wa mbali katika jengo hilo la kanisa
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akivikwa skafu maalum wakati alipowasili kwenye uwanja wa CCM Kilumba katika sherehe za kufunga Jubilee ya miaka 50 ya kanisa hilo Jijini Mwanza.
Heshima zikitolewa kwa mgeni rasmi
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakishuhudia matembezi ya sherehe hizo
Matembezi ya sherehe hiyo yakiendelea
Sehemu ya umati wa watu katika tukio hilo la Jubilee ya Miaka 50
Vikundi vya matembezi yakiendelea
Jukwaa kuu wakishuhudia matembezi hayo
Vijana wadogo wa Path Finde-(PF) wakipita mbele ya mgeni rasmi kutoa heshima zao. 
Vijana wadogo wa Path Finde-(PF) wakipita mbele ya mgeni rasmi kutoa heshima zao
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akielekea kukagua gwaride la vijana hao
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua gwaride hilo
Sehemu ya wananchi wakishuhudia tukio hilo
Vijana PF wakipita kwa mwendo wa haraka mbele ya mgeni rasmi (Hayupo pichani)
Jukwaa kuu wakishuhudia matembezi hayo

Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angeline Mabula akitoa salamu katika tukio hilo
Vijana wakiwa katika hali ya ukakamavu katika tukio hilo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akihutubia katika tukio hilo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akipokea vitabu kama kutoka kwa uongozi wa kanisa hilo vyenye mafunzo mbalimbali 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akishuka katika jukwaa kuu mara baada ya kumalizika kwa tukio hilo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Jaji Mkuu na Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Mzee Mark Boman.  Mzee Boman ni miongoni mwa Wazee waanzilishi wa kanisa hilo ambalo kwa sasa limetimiza Jubilee ya Miaka 50.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla ateta jambo na Jaji Mkuu na Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Mzee Mark Boman ambaye ni moingoni mwa waaumini wa mwanzo wa kanisa hilo. (Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog-Mwanza).

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.